JINA LA KITABU: Sanaa ya Maombi: Basi Salini Hivi
MWANDISHI: FELICIAN MAKARIOS PHOS
MWAKA WA KUCHAPISHA: 2023
KUHUSU KITABU
Katika kitabu hiki tutakua na ufafanuzi wa kina na wa vitendo juu ya somo na sanaa ya maombi. Kujifunza sanaa ya maombi ni muhimu sana kwa mwenendo wa mkristo. Wanafunzi wa Yesu ikawabidi kusema na Yesu: “tufundishe kuomba”. Maelekezo ya Paulo kwa Timotheo yalikua, “kabla ya mambo yote… maombi”. Yakobo pia anamtumia Eliya kutukumbusha ufanisi wa maombi na maombi endelevu. Petro anakazia hilo hilo kwa kumwambia mwenye haki kuwa anasikiwa na Mungu katika maombi yake. Yohana anamtia moyo mwamini kuomba neno lolote, na Yuda anasema mkijijenga juu ya imani yenu kwa kuomba.
Kanisa la mahali linajengwa juu ya utamaduni wa maombi. Hivyo ni muhimu kujua kwa nini tunaomba, namna gani ya kuomba na tunaomba nini. Hili ni fundisho la Biblia kama ilivyo katika Maandiko. Kitabu hiki kitajikita katika utajiri wa mwamini mwombaji, kuchunguza nguvu iliyomo ndani yake, kutunza mlengo wetu kwa mlengo wa Mungu, kutatua au kuelezea imani potofu na mashaka mbalimbali, na kukufanya uone kila sababu ya kuomba.
Tutajibu maswali mengi pia kuhusu maombi kama vile: nini nafasi ya mwamini katika maombi, Je, kuna kitu kinachoitwa "maombi yasiyojibiwa", “kuomba vibaya”? Mungu husema ndiyo au hapana katika maombi? Na Je, tuna aina tofauti za maombi? Haya na mengine mengi yanajibiwa katika kitabu hiki.