NB: GHARAMA ZA USAFIRI MTEJA ATALIPIA WAKATI WA KUPOKEA AU KUTUMA BIDHAA KULINGANA NA ANUANI ALIYOWEKA
PRE ORDER SALE OFFER
VITABU VITAANZA KUPATIKANA TAREHE 10 OCTOBA 2025
UTANGULIZI:
Nilipogundua kuwa, siwezi kumbadilisha aliyeniumiza kwa kumchukia na kuwa tu na hasira naye, NIKAMSAMEHE.
Bado nikajihisi kuwa nina mzigo. Nilipojichunguza vyema, nikabaini, nikisikia jina lake, naumia. Nikisikia sauti yake naumia. Nikimuona naumia. Nikajiuliza, ni nini hiki? Ndipo nikagundua nimembeba, anaishi kwenye kile kidonda alichosababisha, nikafanya uamuzi wa KUMUACHILIA.
Kwakuwa msamaha ni mchakato na mara nyingine huchukua muda, nikaanza kuhisi nilichelewa kuchukua hatua. Nikaanza kujilaumu kwa nafasi nilizotoa zilizozidisha makovu. Nikaanza kujichukia na kutamani kujiadhibu. Lakini, kabla hali haijawa mbaya, nikajisahili, Je! Si rahisi zaidi kujisamehe binafsi kuliko kumsamehe mwingine? NIKAJISAMEHE.
Siku zote naikumbusha nafsi yangu kuwa, "Msamaha ni zawadi ghali zaidi ninayoweza kuitoa kwa ajili ya ustawi wangu binafsi"
Ungana nami katika KUSAMEHE.